Triple A FM
Triple A FM
13 January 2026, 10:59 am

Na Joel Headman
Wananchi wa kwa Mrombo jiji la Arusha wanatarajia kunufaika na ujenzi wa soko jipya la kwa Morombo ambalo tayari ujenzi wake umeanza.
Wafanyabiashara hao wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 500 waliokuwa wakifanya biashara eneo hilo awali hawakuwa na soko la kisasa ambapo ujenzi wa sasa ukikamilika unatarajiwa kuwa na wafanyabiashara zaidi ya 700
Akikagua maendeleo ya ujenzi wa soko hilo mkuu wa mkoa wa Arusha Amos amewataka wakandarasi wanaotekeleza mradi huo kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa viwango
Pia mkuu wa mkoa ameurai uongozi wa jiji la Arusha kuhakikisha wafanyabiashara wa awali wanapewa kipaumbele katika ugawaji wa maeneo ya biashara (vizimba) kwenye soko hilo INS..Makala