Triple A FM

Uzushi na Uongo hauna nafasi Arusha

21 October 2025, 2:46 pm

Kamishna msaidizi wa polisi Salvas Makweli akizungumza kwenye kipindi cha Jambo Tanzania

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limewataka wananchi kujiepusha kusambaza taarifa za uzushi na uongo hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wan chi uliopangwa kufanyika Oktyoba 29 mwaka huu

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna msaidizi wa polisi Salvas Makweli kwenye kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na redio Triple A fm kila siku Jumatatu-Ijumaa kuanzia saa 12 mpaka 3 asubuhi akimuwakilisha kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo kueleza namna jeshi lilivyojipanga kukabiliana na taarifa potoshi kipindi cha Uchaguzi

SACP Makweli ameeleza kuwa taarifa za uongo zinazoenea kwenye jamii kwa njia tofauti zinakuwa na malengo mbalimbali ambayo jamaa inapaswa kuyajua na kuyaepuka

Kamishna msaidizi wa polisi Salvas Makweli

Amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kutokuwa na hofu juu ya uvumi unaosambazwa mitandaoni kuwa kutakuwa na vurugu siku ya uchaguzi na kuwahakikishia kuwa jeshi la polisi lipo imara kudhibiti hali ya usalama

Kamishna msaidizi wa polisi Salvas Makweli