Triple A FM
Triple A FM
17 October 2025, 7:46 pm

Na Joel Headman
Ndivyo unavyoweza kusema baada ya ushindi wa bao 1 la dakika za jioni walilolipata Fountain Gate dhidi ya Dodoma jiji jioni ya leo
Mchezo huo wa ligi kuu uliopigwa kwenye dimba la Tanzanite Kwaraa umeshuhudia kandanda safi lililotembezwa na timu zote mbili huku kukiwa na mashambulizi ya kupokezana
Kabla ya mchezo huu wa leo Fountain gate walikuwa na kauli mbiu inayosema “Tunaanza na Mungu” n ahata wakati wachezaji wakiingia uwanjani kwa Pamoja na Mashabiki na raisi wat imu hiyo walionekana kusimama na kuimba wimbo wa The Mafik Tunaanza na Mungu mpaka walipokanyaga pictch kisha mashabiki na rais wakapiga makofi na kukaa
Ni kama mchezo ulikua unamalizika bila ya goli kwa pande zote mbili kwani mpaka dakika ya 90 ilikua bila bila na kunako dakika ya 2 kati ya zilizoongezwa ndipo Mudrik Shehe alimalizia krosi safi iliyopigwa kutoka Magharibi mwa uwanja na Jimyson mwinuke na kuiandikia Fountain goli pekee la ushindi
Baada ya mchezo kocha wa Fountain Gate Mohamed Laizer amewashukuru wachezaji na mashabiki kwa namna walivyojitoa na kujipatia ushindi
Kwa upande wa kocha wa Dodoma Jiji Amani Josia amesifu uwezo wachezaji wake licha ya kupoteza na kusema ni sehemu ya mchezo na kuwa watafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza INS….Josia