Triple A FM
Triple A FM
25 September 2025, 1:38 pm

“Kwa sababu mwisho wa siku wale ndio watakuwa mashahidi wako wa kwanza katika…. kuonyesha kwamba umiliki huu ni wa bwana X au ni wa bwana Y”
Na Jolaz Joel Headman
Takwimu rasmi za wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi zinaonyesha kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetatua jumla ya migogoro ya ardhi 18,005 katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024
Licha ya hayo bado takwimu hizo zinaonyesha kuwa hadi kufikia 2021, kulikuwepo na migogoro ya ardhi katika vijiji na mitaa 1,004, ikiwemo vijiji 981 na mitaa 23
Hali hiyo inaonyesha kuwa bado kuna migogoro ya ardhi inayoibuka kutoka maeno mbalimbali nchini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wanachi kutokuwa na uelewa wa kutosha wa sheria ya umiliki wa ardhi Kwa kutambua hilo na kuona malalamiko ya mtandaoni kuhusu migogoro ya ardhi, Triple A fm tumemtafuta mwanasheria Robert Ndomba kutoka ofisi ya wanasheria na mawakili binafsi ya LexVista Attorneys kutoa elimu juu ya mambo ya msingi ya kufanya kabla,wakati na baada ya ununuzi wa ardhi ili kukuepusha kwenye migogoro