Triple A FM
Triple A FM
24 September 2025, 3:04 pm

Na Daudi Peter
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude amewataka wananchi kuwa tayari na kujiandaa kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazoletwa na mashindano ya AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2027
Akizungumza na Triple A Mkude amesema kuwa michuano hiyo imefungua fursa kwa wananchi kujiongezea kipato kwani kutakuwa na muingiliano mkubwa wa watu na hivyo wajiandae kutoa huduma zinazoendana na hadhi ya mashindano hayo
Akizungumza kwa upande wa maandalizi ya uwanja ameeleza kuwa mpaka sasa ni zaidi ya 60% na kwamba mradi huo utakamilika kwa wakati.