Triple A FM
Triple A FM
24 September 2025, 2:35 pm

“Suala zima la riadha,suala zima la mpira wa miguu,mpira wa mikono,mpira wa pete na michezo aina nyinginezo nyingi kwa sababu tunaona fursa ya ajira”
Na Joel Headman
Mgombeau rais wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha United Democratic Party (UDP) bi.Saum Rashid ameahidi kuinua pato la mkoa wa Arusha kupitia utalii wa michezo
Akijibu swali la mwandishi wa Triple A aliloulizwa kwenye mkutano wa kampeni alioufanya jana kituo kikuu cha mabasi Arusha, Bi Saum amesema atashughulikia suala hilo kwa haraka mara tu atakapochaguliwa kuwa raisi.
Kuhusu mapambano dhidi ya rushwa na ukwepaji wa kodi ameahidi kushughulikia suala hilo ikiwemo kuweka mifumo mizuri ambayo haitamuumiza mfanyabiashara na itakuwa inamvutia kulipa kodi kwa hiari