Triple A FM

Ubwabwa ni lugha ya picha-Mgombea CHAUMMA

17 September 2025, 10:36 am

Mgombea ubunge jimbo la Arumeru Magharibi kupitia chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) bi.Nasinyari Mollel

“Nimekuja kupitia kauli yangu ya mimi nitawafikisha,endapo nitapata…endapo nitafanikiwa kuwa mbunge wa jimbo hili”

Na Joel Headman

Mgombea ubunge jimbo la Arumeru Magharibi kupitia chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) bi.Nasinyari Mollel ameeleza kuwa sera inayopigiwa chapuo na chama chake ya “Ubwabwa” ni lugha ya picha inayoakisi mabadiliko ya maisha kwa Watanzania

Akizungumza mkoani Arusha Bi Nasinyari ameeleza kuwa sera hiyo na nyingine zinalenga kubadilisha maisha ya Watanzania hasa wa Jimbo lake kutoka changamoto wanazopitia sasa na kuona mabadiliko

Mgombea ubunge jimbo la Arumeru Magharibi kupitia chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) bi.Nasinyari Mollel

Amegusia pia sula la elimu na afya na kueleza mambo ambayo atayafanya iwapo atachaguliwa.

Mgombea ubunge jimbo la Arumeru Magharibi kupitia chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) bi.Nasinyari Mollel

Mgombea huyo anatarajiwa kuzindua kampeni zake za ubunge Jumamosi tar. 20-09-2025 eneo la ofisi ya kijiji cha Oloigeruno kata ya Ilkiding’a Jimbo la Arumeru Magharibi