Triple A FM
Triple A FM
31 July 2025, 10:50 am

“Akasema mama wawili nifungulie huku kwako nilale, mama wawili akasema we lala tu mbona hamna watu? Mama wawili yeye akalala Rasi kumbe kamtumia meseji…
Wananchi wa mtaa wa Olmokea kata ya Sinoni Mkoani Arusha wameeleza kugubikwa na hofu kufuatia matukio yanyotokea kwenye maeneo yao kwa nyakati tofauti.
Hio ni kutokana na kupatikana kwa mwili ulioning’inia mtini kwenye mtaa huo ambapo baadae uligundulika kuwa ni wa Kijana Bosco Massawe (Rasta) ambaye amekuwa akiishi jirani na eneo ulipokutwa siku ya Jumanne Julai 30.
Mwili huo umepatikana ukiwa na majeraha mbalimbali pamoja na michirizi ya damu barabarani kuelekea kwenye eneo hilo hali iliyozua sintofahamu kwa wananchi
Watu wa karibu wameelezea namna walivyomfahamu Bosco mna jinsi walivyoguswa na msiba wake.
Kukutwa kwa mwili huo ni tukio la 2 la hivi karibuni baada ya lile lililotokea mwisho wa wiki July 27 la kukutwa kwa mwili wa motto Mishel Amani miaka miwili na nusu uliokuwa umetupwa kwenye mto Naura baada ya kupotea kwa siku 1 Triple A fm bado inafanya jitihada za kumpata kamanda wa polisi mkoani apa Justine Masejo kutolea ufafanuzi matukio haya