Triple A FM
Triple A FM
29 July 2025, 10:45 pm

Na Joel Headman Arusha
Nchi ya Tanzania inazidi kung’ara katika medani za kimataifa na kuifanya kushika nafasi za juu katika nchi ambazo uhusiano wake na China unazidi kuimarika.
Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kiraia la Doublethink Lab ambalo limeitoa kwa redio Triple A FM kuelezea kuhusu umuhimu wa serikali ya China kwa nchi ya Tanzania na hatua za kimaendeleo zilizopigwa mpaka sasa kati ya nchi hizo mbili.
Kupitia mradi wake wa kwanza wa uchunguzi wa China Index toleo la mwaka 2024 likihusisha nchi 101 duniani limeitaja Tanzania kushika nafasi ya 19 duniani kati ya nchi zinazoongoza kwa ushawishi kati yake na China.
Viwango hivyo vipya vinaonyesha kuimarika kwa uhusiano wa Tanzania na China kiuchumi na kijeshi ikiwa ni mshirika wake mkuu wa biashara na mshirika wa muda mrefu wa ulinzi na kijeshi.
Katika eneo la utungaji na utekelezaji wa sheria jumuishi na sera za kigeni Tanzania imeshika nafasi ya 9 ikionyesha juhudi za mafanikio za Chama cha Kikomunisti cha China (CCP) kutumia uhusiano wa karibu wa kiuchumi na kanuni za kimataifa
China Index imetumia viashiria 99 kuchambua viwango hivyo ambavyo ni pamoja na Vyombo vya habari, Elimu ya juu, Uchumi na vinginevyo. China In The World (CITW) ni mtandao wa kimataifa ulioanzishwa 2019 ili kusaidia watafiti wanaochunguza ushawishi na propaganda za China duniani kwa kushirikiana na shirika la kiraia la Doublethink Lab