Triple A FM
Triple A FM
31 May 2025, 6:53 pm

Na Joel Headman Babati
Ushindi wa 3-1 dhidi ya Simba ni kama umewapa mzuka sana Singida United aisee
Mnyama Simba sasa hana lake tena kwenye mashindano ya shirikisho Tanzania kwani kwa kipigo hicho wameaga rasmi mashindano hayo
Mechi hii ni kama ya kulipa kisasi kwa Simba baada ya kupata ushindi wa 1-0 Dar Es Salaam ushindi ambao ulilalamikiwa
Akizungumza Kocha wa Singida BS David Ouma amesema si mara ya kwanza Kuifunga Simba na kuwa ataendelea kuwafunga vigogo wa soka nchini
Kwa upande wa Fadlu Davis wa Simba ameshukuru wachezaji kwa uwezo wa kujitoa na kuwa hawezi kulalamikia ratiba ya michezo ambayo hata hivyo sio rafiki