Triple A FM

Arusha tayari kwa msimu wa utalii

30 May 2025, 1:03 pm

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP William Mkonda

Na Joel Headman

Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha limewakutanisha zaidi ya madereva 800 wanaoongoza watalii kwa ajili ya kuwapatia mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo pindi wanapotoa huduma hiyo ya usafiri

Akifungua mafunzo hayo mkoani Arusha, kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP William Mkonda amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbusha madereva sheria na kanuni za usalama barabarani pamoja na kujadiliana changamoto wanazokumbana nazo ili kuona namna bora ya kuzitatua

SACP Mkonda amebainisha kuwa Madereva wanaobeba watalii ni watu wa muhimu katika kuhakikisha usalama wa wageni

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP William Mkonda

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa Waendesha Watalii Nchini (TTGA) Lembrisi Moses amesema jumla ya madereva 800 wameshiriki katika mafunzo hayo yaliyowakumbusha wajibu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani

Mwenyekiti wa Waendesha Watalii Nchini (TTGA) Lembrisi Moses

Kwa upande wake Usia Israel ambaye ni dereva wa watalii amesema kupitia mafunzo hayo amekumbushwa namna ya kuwa na udereva wa kujihami pindi awapo barabarani INS…

Dereva wa utalii Usia Israel