Triple A FM

Kilio cha shule kata ya Sakina

27 May 2025, 10:55 am

Diwani wa Kata ya Sakina Elvicent Willson wakati wa mahojiano

Na Jane Silayo

Diwani wa Kata ya Sakina Mkoani Arusha ameiomba serikali kuwajengea shule ya sekondari ndani ya kata hiyo ili kuchochea maendeleo ya elimu kwa watoto.

Akizungumza katika Kipindi cha Ukurasa Mpya cha Triple A Radio, Bw Elvicent Willson Fadhili amesema kuwa wazai na walezi wa kata hiyo wanatumia gharama kubwa kuwapeleka watoto shule za mbali hali inayowaumiza kiuchumi.

Ameeleza kwamba licha ya kuwa na uhitaji wa shule ya msingi na sekondari, kwa sasa wanahitaji Zaidi ya sekondari ambapo wanafunzi wakifaulu wanapangiwa mbali.

Diwani wa Kata ya Sakina Elvicent Willson akizungumzia suala la shule

Akizungumzia fursa za mikopo ya ya asilimia 10 kwa vijana,kina mama na wenye ulemavu inayotolewa na halmashauri amewataka vijana kuwa wavumilivu ili kupata mikopo hiyo ambayo inatumia mchakato wa muda mrefu kuipata.

Diwani wa Kata ya Sakina Elvicent Willson akizungumzia mikopo