Triple A FM

Makonda achagua Jimbo la Arusha Mjini

21 May 2025, 10:29 am

Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda akikagua kitambulisho chake cha kupigia kura

Na Joel Headman

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amewahamasisha wananchi kujitokeza kuhakiki taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura

Ametoa hamasa hiyo Jumatatu Mei 20, 2025 kwenye kituo cha kuandikisha wapiga kura kilichopo kwenye Hospitali ya AICC, Mtaa wa Mahakama Kata ya Sekei Jimbo la Arusha mjini ambapo amechagua kuwa kituo chake cha kupigia kura mwezi Oktoba

Makonda ameeleza kuwa ili mwananchi aweze kushiriki zoezi zima la kuchagua viongozi anaowataka ni lazima awe amehakikiwa taarifa zake

Mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda

Uhakiki wa taarifa za wapiga kura mkoani Arusha unafanyika kwa awamu ya pili ambayo inatarajiwa kukamilika Mei 22 ambapo itatatoa nafasi kwa wananchi waliojiandikisha kupiga kura ya kuchagua viongozi katika ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani mwezi Oktoba 2025