Triple A FM
Triple A FM
18 May 2025, 6:00 pm

Na Joel Headman
Saa chache baada ya kupatikana kwa mchungaji wa kanisa la huduma ya Kristo lililopo Kata ya Muriet mtaa wa FFU mkoani Arusha Steven Jacob, mapya yameibuka leo kanisani kwake
Ibada ya leo Jumapili iliyofanyika kanisani hapo, imeshuhudiwa ikiongozwa na mchungaji Vulfrida George badala ya mchungaji Steven.
Katika mahubiri hayo mchungaji Vulfrida ameeleza kuwa bado wana Imani kubwa kwa Mungu kuwa anaweza kufanya mambo yanayoonekana hayawezekani.
Ameeleza kuwa kanisa linaendelea kufanya maombi kwani ndio yanaweza kuwashindia katika hali wanayopitia
Mchungaji Steven Jacob anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana Ijumaa ya wiki hii mei 16 kabla ya baadaye kupatikana wilayani Siha mkoani Kilimajaro.
Hata hivyo baada ya kupatikana siku ya Jumamosi Mei 17 amezungumza na waandishi wa habari na kuelezea yaliyomkuta.
Wakati akielezea kupotea kwa mwanae, baba mzazi wa mchungaji huyo Jacob Gumbo ambaye pia ni balozi wa nyumba 10 kwenye eneo hilo amekemea matendo maovu yanayofanywa kwa watumishi
Bado tunaendelea kutafuta jeshi la polisi mkoani hapa kuhusu uthibitisho wa tukio hili na kinachoendelea mpaka sasa