Triple A FM

Waongoza watalii walilia miundombinu ya barabara

13 May 2025, 10:39 am

Waongoza watalii wakiwa mbugani (Picha na mtandao)

Waongoza utalii wamepaza sauti juu ya ubovu wa miundombinu ya barabara ambayo imekuwa ikiwarushisha nyumba katika shughuli zao za utalii wawapo mbugani

Na Joel Headman

Wadau na wanachama wa chama cha waongoza watalii Tanzania TTGA wameiomba serikali kushughulikia suala la miundombinu mibovu inayochangia kurudioisha nyuma sekta ya utalii nchini.

Ombi hilo limetolewa kwenye mkutano wa mwaka wa TTGA Uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na watu mbalimbali kwa lengo la kujadili maendeleo ya sekta hiyo muhimu ya mapato nchini.

Akizungumza katibu mkuu wa TTGA Robert Maxi ameeleza kuwa barabara zinapokuwa mbovu zinatengeneza ugumu kwa waongozaji kufanya kazi hiyo

Sauti ya Robert Maxi

IKufuatia hali hiyo wamesema kuwa ili kupata mafanikio zaidi kwenye sekta hiyo marekebisho ya miundombinu ni muhimu.

Akihutubia mkutano huo mkuu wa kitengo cha utalii kutoka mamlaka ya usimamizi wa hifadhi za taifa nchini (TANAPA) Bi Jully Lyimo amewataka waongoza watalii kutoa kipaumbele kwa taifa na kulitangaza vyema kwa kuwa na uzalendo kwa nchi yao.

Sauti ya Jully Lyimo