Triple A FM

Ujumbe wa marehemu wazua ‘Utata’ Arusha

1 October 2024, 8:25 pm

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha SACP Justine Masejo

Na Joel Headman Arusha

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linafanya uchunguzi wa kifo cha mtu mmoja mkazi wa Baraa jijini Arusha aliyekutwa msituni akiwa amening’inia juu ya mti.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna msaidizi wa Polisi Justine Masejo amemtaja marehemu kuwa ni David Mollel mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati ya miaka 50 hadi 55.

Mwili huo umekutwa eneo la mlima Oldonyomasi uliopo kata ya Moivaro Jijini hapa pamoja na ujumbe uliotajwa kuwa ni ‘tata’ uliotumwa kwa ndugu zake jana Sept 30 ambao hata hivyo haujawekwa hadharani.

Licha ya uchunguzi unaohusisha jeshi la polisi na taasisi nyingine kuendelea, Kamanda Masejo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha Mount Meru