Triple A FM

Onyo kali latolewa kwa wakuu wa mikoa

28 September 2024, 11:14 am

Na Joel Headman Babati

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewatahadharisha wakuu wa mikoa nchini kufikiria mara mbili mbili namna watakavyoingia mkoani Manyara.

Wakuu wa mikoa waliopewa onyo hilo ni wale wote wenye timu za ligi kuu kwenye mikoa yao akiwataka kusindikiza timu zao ili zisiishiwe nguvu zinapokwenda kucheza wilayani Babati.

Jeuri ya RC Sendiga haiji hivi hivi ila inaletwa na timu yake ya Fountain Gate ambayo imeugeuza uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati kuwa machinjio ya timu za ligi kuu kwani haijapoteza mchezo wowote kwenye uwanja huo toka ilipotangaza rasmi kuwa uwanja wake wa nyumbani.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akizungumza na Waandishi wa habari

Onyo lake amelitoa uwanjani hapo baada ya FG kuwashushia kipigo kizito cha 3-1 walima miwa wa Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa jana jioni.

RC Sendiga