DSW yakutanisha wadau kuimarisha mifumo ya kuzuia ukatili wa kijinsia.
2 May 2024, 4:48 pm
“Arusha inaonekana inaongoza katika matukio ya ukatili kwa sababu matukio mengi yanaripotiwa tofauti na mikoa mingine nchini”
Na.Anthony Masai.
Shirika lisilo la kiserikali la DSW lenye makao yake makuu mkoani Arusha linalotekeleza mradi wake wa SAFA wenye lengo la kuwezesha vijana kuboresha maisha yao katika maeneo ya afya,elimu,kipato na ustawi ili kufikia malengo yao,kwa kushirikiana na Serikali limekutanisha wadau kujadili na kuweka mikakati ya kuimarisha mifumo ya kuzuia ukatili wa kijinsia.
Afisa Maendeleo ya jamii Mkuu,Wizara ya Maendeleo ya jamii,jinsia,wanawake na makundi maalum,Christabela Ngowi akizungumza na waandishi wa habari pembezoni mwa kikao hicho,ameilishukuru Shirika la DSW kwa jitihada zake za kushirikiana na Serikali katika mipango mbalimbali inayohusu vijana na kwamba Serikali inaendelea na kampeni za kuifikia jamii kupitia mifumo ya kuzuia ukatili wa kijinsia nchini.
Akizungumza kuhusu kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika katika makao makuu ya DSW yaliyopo Tengeru,Arusha;Mratibu wa Miradi wa shirika hilo Celina Protas amesema mifumo ya kuzuia ukatili wa kijinsia inahusisha makundi mbalimbali ya watu katika jamii.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Arusha,Brandina Nkini amepongeza jitihada zinazofanywa na vyombo vya habari na jamii ya watu wa Arusha kwa kuwa mstari wa mbeleo kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Jeshi la polisi kupitia kwa Mkaguzi wa Polisi ambaye pia ni Polisi kata ya Kiutu Tunu Makwaya amezungumzia changamoto ambazo bado zinawakabili katika kukabiliana na vitendo ukatili wa kijinsia katika jamii wanazofanyia kazi.