madiwani wapitisha bajeti kuboresha jiji la Arusha
7 March 2024, 3:54 pm
“vipaumbele vitakuwa katika sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu kwani maeneo hayo ndio yanawagusa wananchi moja kwa moja”
Na.Anthony Masai
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Arusha limepitisha Bajeti ya kiasi cha shilingi Bilioni 51 kutoka katika mapato ya ndani kwa mwaka 2024/2025,ikilenga kufunga taa za Barabara katika Jiji lote, kuboresha masoko,kujenga uwanja mdogo wa mpira wa miguu na kununua timu ya mpira wa miguu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranqe amesema,vipaumbele vitakuwa katika sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu kwani maeneo hayo ndio yanawagusa wananchi moja kwa moja.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini amesema,wamejipanga kuongeza makusanyo ya mapato kutoka vyanzo vyake mbalimbali ikiwemo kodi za upangishaji wa maduka na Masoko.