Mtegani FM

Makunduchi yatarajia kupata uwanja wa ndege na helikopta

22 October 2026, 12:38 pm

Picha ikionesha eneo ambalo linarajiwa kujengwa uwanja wa ndege makunduchi, Picha na Miraji Manzi Kae

Serikali inatarajia kujenga uwanja mdogo wa ndege katika eneo la Makunduchi, utakaokuwa na uwezo wa kuhudumia ndege za abiria za ukubwa wa kati na mkubwa (daraja la 3C), zikiwemo zile zinazobeba kuanzia abiria 72 hadi zaidi ya 150 kwa wakati mmoja

Na Hafsa Ali Idrissa

Uwanja huo unatarajiwa kuwa na miundombinu ya kisasa itakayowezesha kutua kwa ndege kubwa za mashirika ya kimataifa kama vile Flydubai na Oman Air

Akieleza mchanganuo wa mradi huo, mtaalamu wa ujenzi ameeleza kuwa uwanja huo utakuwa na eneo la kurukia na kutulia (runway), njia ya kuunganishia ndege kwenda eneo la maegesho (taxiway), eneo maalum la kuegeshea ndege (apron), pamoja na jengo la kisasa la abiria (terminal building)

Hali kadhalika, mradi huo unahusisha pia ujenzi wa maeneo manne maalum ya kutua na kurukia helikopta (helipads) katika maeneo ya Makunduchi, Lumumba, Fumba, Kizimkazi na Paje.

Sauti ya Mkandarasi Akieleza mchanganuo wa mradi huo

Kila eneo la helipad litakuwa na ukubwa wa mita 40 kwa 40, likiwa na unene wa saruji wa milimita 200 (thickness), uliosanifiwa maalum kuhimili helikopta kubwa zenye uwezo wa kubeba hadi abiria 19

Mradi huo utawekewa mfumo na huduma zote muhimu zitakazowezesha viwanja hivyo kufanya kazi masaa 24, mchana na usiku, ili kuimarisha sekta ya usafirishaji na utalii kisiwani humo.