Mtegani FM

Tadio yatoa mafunzo kwa waandishi wa Mtegani FM Radio

12 December 2024, 11:18 pm

Mhariri wa Radio Tadio Hilali Ruhundwa (Aliyenyoosha kidole) akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Radio Mtegani FM. Picha na Saumu Ali Haji

Watangazaji na waandishi wa habari wa radio jamii Mtegani FM Makunduchi Zanzibar wametakiwa kutumia kalamu zao vizuri kuandika na kuripoti habari za uchaguzi 2025.

Na Miraji Manzi Kae

Mafunzo hayo yametolewa na mhariri wa jukwaa la kupashana habari la Radio Tadio lililo chini ya Taasisi ya Muunganiko wa Radio Jamii Tanzania TADIO Bwana Hilali Alexander Ruhundwa katika mafunzo kwa waandishi na watangazaji ikiwa lengo ni kuwafungua wanahabari kuandika habari bila ya kubagua vyama na hali za watu.

Ameongeza kwa kusema kuwa kupitia mafunzo hayo anaamini waandishi wataandika habari ambazo zina weledi bila ya kubagua chama wala mtu wa chama fulani.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia katika kuandika habari zao vizuri hasa katika kuelekea katika uchaguzi 2025.

sauti ya mshiriki wa mafunzo.