Mtegani FM

Tadio yatoa mafunzo kwa waandishi wa Radio Mtegani

12 August 2023, 3:22 pm

Mhariri wa Radio Tadio Hilali Ruhundwa ( Alienyoosha kidole ) Akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa ridio mtegani. Picha na Ramadhani Bilali

Watangazaji na wandishi wa habari wa radio jamii Mtegani Fm Makunduchi Zanzibar wametakiwa kutumia mtandao wa Radio Tadio ili kuifikia jamii kimataifa.

Na Fatma Saleh

Ushauri huo umetolewa  na mhariri wa jukwaa la kupashana habari la Radio Tadio lililo chini ya Taasisi ya Muunganiko wa Radio Jamii Tanzania TADIO Bwana Hilali Alexander Ruhundwa katika mafunzo kwa waandishi na watangazaji ikiwa ni mwendelezo  wa mafunzo hayo na kuwafungua wanahabari ili wawe mbele kiteknolojia.

Hata hivyo ameongezea kwa kusema kuwa kupitia mtandao huo kuanzia leo  habari zao hazitosikika hapa Kusini Unguja tu bali zitasikika  na kuonekana dunia nzima baada ya kuchapishwa kwenye mtandao tofauti na hapo awali.

Sauti ya Mhariri wa Radio Tadio Tanzania Hilali Ruhundwa

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo  yatawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo utumaji wa habari kimtandao.

Sauti Ya Mshiriki Rashid Ramadhan