Wanawake watakiwa kushiriki katika kamati za michezo
25 November 2024, 11:29 am
‘Kamati’ ni neno linalotumika kumaanisha kikundi cha watu wanaokusanyika kwa kusudi maalum. Kwa kawaida, kamati inaweza kuwa na majukumu mbalimbali, kama vile kupanga na kufanya maamuzi, kusimamia shughuli za shirika au kampuni, au kufanya uchunguzi kuhusu jambo fulani. Kwa mfano, kamati ya fedha inaweza kusimamia matumizi ya pesa katika shirika, na kamati ya maendeleo inaweza kufanya mipango ya kuboresha huduma au miradi.
Na Mwiaba Kombo
Mara nyingi katika jamii yetu imekuwa tofauti kabisa wanawake kuchaguliwa katika kamati za michezo lakini ni tofauti kabisa kwa baadhi ya wanawake .Makala maalum ambapo kwa siku ya leo tutazungumzia Ni kwa kiasi gani wanawake wanashirikishwa katika kamati za michezo kisiwani Pemba ambapo Makala hii inaletwa kwako na Mwiaba Kombo Hamad, kwa ushirikiano wa Chama Cha Waandishi Wa Habari Wanawake, Tanzania, Zanzibar (TAMWA Zanzibar) kupitia mradi wa Michezo kwa Maendeleo unaotekelezwa chini ya ufadhili Taasisi ya Maendeleo ya Mashirikiano ya Ujerumani (GIZ) nikusihi tuwe pamoja mwanzo hadi mwisho wa Makala hii.