Micheweni FM

Wanawake watakiwa kuzigeuza changamoto kuwa fursa michezoni

25 November 2024, 10:57 am

Mchezaji wa simba queens kutoka nchini kenya akiwa kwenye majukumu yake ya timu ya Taifa.

Changamoto ni mazingira kinzani ya upinzani kwenye kila nyanja yanayokuja katika maisha yako ambapo kwa jina jengine tunaiita matatizo ambalo neno hili ni baya kwa watu wengi katika jamii neno hili linajumuisha matatizo ya kiuchumi ,kijamii na kisiasa ,lakini leo tutazungumza Zaidi changamoto kwenye jamii katika suala zima la michezo .

Na Mwiaba Kombo.

Makala maalum ambapo kwa siku ya leo tutazungumzia  changamoto ambazo wanakumbana nazo wanawake katika suala la michezo  Mkoa wa kaskazini  Pemba ambapo Makala hii inaletwa kwako na Mwiaba Kombo Hamad, kwa ushirikiano wa Chama Cha Waandishi Wa Habari Wanawake, Tanzania, Zanzibar (TAMWA Zanzibar), kupitia mradi wa Michezo kwa Maendeleo unaotekelezwa   chini ya ufadhili shirika la Maendeleo la Nchini Ujerumani (GIZ)  nikusihi tuwe pamoja mwanzo hadi mwisho wa Makala hii