Micheweni FM
Micheweni FM
18 July 2025, 10:48 am

Shule za shumba vyamboni masingi Tumbe na Tumbe Sekondari ni miongoni mwa shule ambazo zilikuwa na kilio cha muda mrefu wa kupata huduma ya fotokopi kwa ajili ya kutolea mitihani ya wanafuni pamoja na shughuli nyengine za kiofisi ,kilio hicho kimepata ufumbuzi baada ya mbunge wao wa jimbo hilo kuweza kuwapelekea mashine hizo ambazo zitatumika kwa matumizi ya ofisi.
Na Mwiaba Kombo
WALIMU wa skuli za shumba vyambo msingi ,tumbe msingi na Sekondari wametakiwa kuzitumia mashine za fotokopi ambazo wamepewa kwa lengo la kurahisisha kazi zao ili wanafunzi wapate kuafaulu vizuri .
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mbunge wa jimbo la Tumbe Amour Khamis Mbarouk amewataka walimu kuhakikisha kwamba lengo la fotokopi hizo zinatumika kama ambavyo imekusudiwa
Kwa upande wake mwenyekiti wa skuli ya shumba vyamboni msingi Salim Khamis Abdalla wameahidi kuvitunza vifaa hivo na kuvitumia kama ambao imekusudiwa kwani kilikuwa ni kilio cha muda mrefu kwao.
Wakitoa neon la shukrani mwalimu mkuu skuli ya Tumbe Sekondari Asha Rashid Abdalla pamoja na mwalimu mkuu skuli ya shumba vyamboni msingi Seif Khamis Ali wamempongeza mbunge mstaafu huyo kwa kuweza kuwatatulia kilio cha muda mrefu ambacho kilikuwa kikiwakabili katika skuli zao.