Micheweni FM
Micheweni FM
29 June 2025, 4:17 pm

Ni zaidi ya miaka minne katika kijiji cha kwa pengo shehia ya Sizini wameendelea kukosa huduma ya maji safi na salama ambapo ni jambo la msingi na muhimu kwa matumizi ya binadamu ya kila siku .
Na Fatma Faki
WANANCHI wa kijiji cha kwa Pengo, shehia ya Sizini wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba wamelalamika juu ya ukosefu wa huduma ya Maji safi na salama katika kijiji chao.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao wamesema huu ni zaidi ya mwaka wa nne, hawapati huduma ya maji safi na salama kijijini humo.
kwa upande wake afisa wa mamlaka ya maji safi na salama (ZAWA) Yusouf Ali Faki amesema ongezeko la watu katika vijiji ndio sababu kubwa ambayo inapelekea baadhi ya vijiji kukosa huduma hiyo.