Wadau wa afya wakumbushwa kufikisha elimu ya afya sahihi kwa jamii
23 November 2023, 4:47 pm
Na Mwiaba Kombo
Wadau wa afya kisiwani Pemba wametakiwa kufikisha taarifa sahihi Kwa jamii kuhusiana na maradhi ya mripuko kutokana na mvua ambazo zinazoendelea kunyesha.
Ushauri huo umetolewa na Afisa mdhamin wizara ya Afya Pemba Khamis Bilali Ali wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya siku Moja katika ukumbi wa Sammail Gombani? Chake chake Pemba juu ya kutoa taarifa sahihi Kwa jamii kuhusu maradhi hayo .
Amesema mara nyingi kipindi Cha mvua kunaakuwa na uvumi /tetesi kuhusu magonjwa mbalimbali ya kuambukiza Kwa jamii zisizo na ukweli ndani yake hivyo ni vyema Kila Mmoja Kwa nafasi yake kuhakikisha kuwa anafikisha elimu hiyo kwa jamii na Kwa usahihi.
Amewataka washiriki hao kuhakikisha wanajitoa kwa hali na mali kufikisha elimu kwa jamii ili iweze kuwa na uelewa juu ya madhara ambayo yanaweza kujitokeza hususan kipindi hiki cha mvua
Kwa upande wake mkuu wa kitengo Cha Elimu ya afya Zanzibar Hamad Hamad Magarawa amesema ni muhimu kutoa taarifa zilizo sahihi Ili jamii ipate kile kilicho sahihi na ibaki katika Hali y usalama.
Magarawa amewaomba washiriki hao kuendelea kushirikiana kwa pamoja ili taarifa ziweze kufika kwa jamii husika bila ya kuwepo na athari yeyote.
Akiwasilisha mada juu uvumi (tetesi )ambao unatokea mitaani mwakilishi kutoka shirika la afya duniani (WHO) Juliath Rangi amesema taarifa hizo mara nyingi zinakuwa hazina ukweli wowote hivo ni muhimu kuhakikisha jamii inapewa elimu ya kutosha juu ya uvumi huo.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru wizara ya Afya kupitia kitengo Cha Elimu ya Afya Kwa kuwapatia Elimu hiyo na kuahidi kuifikisha Kwa jamii Kwa usahihi.
Mafunzo hayo ya siku Moja yamewashirikisha waandishi wa habari mbali mbali kutoka Pemba ,wahudumu wa afya wa kujitolea (C.H.V)mafunzo ambayo yameandaliwa na wizara ya Afya Kwa kushirikia na shirika la afya duniani (WHO)wenye lengo la kutoa Elimu kwa jamii.