Tamwa Pemba yawapiga msasa wanahabari juu ya kuripoti habari za udhalilisha
3 November 2023, 7:48 pm
Udhalilishaji ni kumfanyia mtu kitendo chochote kile kitakachomuathiri utu wake na heshima yake na kikamuathiri kimwili na kisaikolojia.
Na Mwiaba Kombo
Waandishi wa habari kisiwani Pemba wametakiwa kutumia kalamu zao na kupaza sauti zao kwa lengo la ukuweza kwatetea waathirika wa matukio ya udhalilishaji .
Kauli hiyo imetolewa na mratibu wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar ofisi ya Pemba Fat-hiya Mussa Said wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuripoti habari za udhalilishaji.
Amesema waandishi wa habari wanayo nafasi ya kufanya ushawishi na utetezi kuhusu athari za udahliulishaji pia kuzungumzia namna waathirika wa matukio haya wanavopata changamoto katika kutafuta haki zao ambazo zimevunjwa .
Aidha ameongeza kuwa waandishi wa habari wanayo nafasi ya kuhakikisha jamii imekuwa na uelewa mzuri juu ya dhana mzima ya udhalilishaji.
Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo Siti Habibu Mohammed ambae ni mwanaharakati kutoka shirika la msaada wa kisheria (ZALHO)amesema pamoja na kuwepo kwa sheria zinazotoa muongozo na adhabu juu ya makosa ya watendaji wa makosa ya udhalilishaji bado vitendo hivi vikiendelea siku hadi siku.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wameahidi kuyatumia vizuri mafunzo hayo kwa lengo la kuhakikisha wanaendelea kuielimisha jamii juu ya athari za udhalilishaji.
Wamesema ni jukumu lao sasa kuona jamii imekuwa na mwamko juu ya kuyaripoti matendo hayo katika sehemu husika ili waaathirika waweze kupata haki zao ambazo wanastahiki.
Mafunzo hayo siku moja yamefanyika katika ukumbi wa chama chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA Zanzibar chake chake Pemba na kuwashirikisha waandishi wa habari 15 kutoka vyombo mbali mbali kisiwani Pemba.