UWT Taifa wampa kongole mwakilishi Zawad wa Konde
27 October 2023, 9:02 am
Umoja wa wanawake Tanzania UWT taifa umeandaa utaratibu wakutembelea miradi mbali mbali ambayo inafanywa na Serikali ya Tanzania pamoja na ya Zanzibar lengo likiwa ni utekeleaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025 ya CCM kwa wananchi juu ya kuwapelekea maendeleo katika maeneo yao.
Na Mwiaba Kombo
Wananchi kisiwani Pemba wametakiwa kuendelea kuunga mkono juhudi zinazoendelea kufanya na dokta Mwinyi pamoja na dokta Samia kwa juhudi za maendeleo ambazo wanaendelea kuwapatia wananchi siku hadi siku .
Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa baraza kuu na mjumbe wa kamati tekelezaji UWT taifa Fatma Salim Abdalla (SUFA) wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa jimbo la konde wakati wa ziara ya umoja wa wanawake mkoa wa kaskazini pemba .
Amesema kazi ambayo inafanywa na marais hawa wawili ni ya kupigiwa mfano ,hivo ni jukumu la wananchi kuendelea kutoa mashirikano kwa viongozi wao ili waweze kuwaletea maendeleo nchini.
Aidha amewataka akina mama kuwaegemeza watoto katika elimu kwani elimu ndio uti wa mgongo wa maisha na kuendelea kutunza mazingira ambayo yamewazunguka katika maeneo yao.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati tekelezaji UWT taifa ambae pia ni mbunge viti maalum mkoa wa Pwani Subira Mgalu amesema lengo la ziara hiyo ni kuanagalia juhudi za maendeleo ambazo zinafanywa na marais wote wawili .
Mgalu amesema baada ya kumaliza ziara hiyo wataeka kongamono kubwa ambalo ni lengo lake ni kuendelea kumpongeze dokta Mwinyi kwa kazi kubwa ya miaka mitatu ya urais wake aliyoifanya.
Ameeleza kufrahishwa na utendaji kazi mzuri ambao unafanywa na wakandarasi ambao wanajenga skuli mbili za ghorofa Konde na Kifundi na kuwaomba kazi ifanyike kwa nguvu na kumaliza kwa wakati.
Nae mwakilishi wa jimbo la Konde Zawad Amour Nassor amesema suala la elimu katika jimbo lake kwasasa anajivunia kuwa na skulinne za ghrofa.
Mjumbe wa kamati tekelezaji mkoa wa kaskazini Pemba ambae pia ni afisa elimu sekondari Tarehe Khamis Hamad amewataka wananchi kutobeza maendeleo ambayo yanafanywa na viongozi hao.
Jumla ya majimbo 9 mkoa wa kaskazini Pemba yametembelewa na kukaguliwa miradi mbali mbali katika majimbo hayo ambapo ziara hii ni ujumbe kutoka UWT taifa wakiongozwa na mwenyekiti Ndg Mary Chatanda pamoja makamu mwenyekiti Bizainab Shomar.