Viongozi wa dini Pemba watakiwa kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa lishe
24 October 2023, 10:09 am
Lishe ni jambo muhimu kwa binadam hivo ni jukumu la kila binadamu kuhakikisha anapata lishe iliyobora ili kujenga mwili imara na madhubuti.
Na Essau Kalukubila.
Viongozi wa dini kisiwani Pemba wametakiwa kutumia nafasi zao kufikisha Elimu ya Lishe kwa jamii ili kujikinga na maradhi mbali mbali ikiwemo upungufu wa damu na Lishe duni.
Wito huo umetolewa na msaidizi mkuu wa kitengo cha Elimu ya Afya Pemba Suleiman Faki Haji wakati akizungumuza na viongozi wa dini na walimu wa madrasa katika mkutano wa siku moja ulioandaliwa na Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Zanzibar.
Amesema viongozi wa dini wananafasi kubwa katika jamii kwani nikundi ambalo linasikilizwa zaidi hivyo ni vyema kuitumia nafasi hiyo katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa lishe.
Akifungua mkutano huo Mratibu wa ofisi ya Mufti Pemba Sheikh Said Ahmed Mohamed amesema Elimu ya Lishe ni muhimu Kwa jamii yote kwani kuna maradhi nyemelezi yanayo muathiri mtu bila kujua na kupelekea kushindwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo kutekeleza ibada
Kwaupande wao washiriki wa mafunzo hayo wameahidi kuitoa elimu hiyo kwenye jamiii ili jamii iweze kuwa na uelewa kuhusu ulaji Mzuri wa vyakula katika jamii