Micheweni FM

PACSO yawapiga msasa wadau juu ya kuilinda haki za bindamu

13 October 2023, 2:55 pm

Mwenyekiti wa PACSO Mohd Ali Khamis akifunga mafunzo ya siku nne kwa wadau wa haki za binadmu katika ukumbi wa chuo cha mbadadala vitongoji chake chake Pemba (picha na Mwiaba Kombo)

Binadamu yeyote duniani ana haki ya kupata kile ambacho anastahili kupata bila ya kuwepo na ubaguzi wowote haijalishi ni mlemavu au sio mlevu , bila kujali ukabila wake ,dini yake ama rangi yake

Na Mwiaba Kombo

Wadau wa haki za binadamu wametakiwa kubadilika katika utendaji wa kazi zao baada ya kupatiwa mafunzo ya kujengewa uwezo juu ya umuhimu wa haki za binadamu .

Akifunga mafunzo hayo mwenyekiti wa Umoja wa Jumuiya zisizo za kiserekali za Pemba (PACSO) Mohd Ali Khamis amesema ipo haja kwasasa kushirikiana kwa pamoja katika kufanya kazi hii .

Amesema katika jamii kumekuwa na changamoto kubwa ambazo zipo hivo ni jukumu la wadau wa haki za binadamu kuhakikisha wanaziibua na kuweza kuzisemea kwa mamlaka husika na mwisho wake kupatiwa ufumbuzi .

Nae mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka kutoka Shirika la Msaada na Haki za Binaadamu Siti Habib Mohamed amesema  kuwa, moja ya haki kuu ya msingi kwa kila mwanadamu ni ile ya kuishi, hivyo ni kosa kwa mtu mwengine yeyote kumuondolea haki hiyo mwenzake.

Hivo amewataka wadau hao kuhakikisha wanaifikisha elimu hiyo kwa jamii husika ili jamii iweze kujua kwa kina haki zao za msingi ambazo ni wajibu wao kuzipata .

Kwa upande wake mtoa mada  Gaspery Charles kutoka Chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA Zanzibar ofisi ya Pemba amewataka waaandishi wa habari katika mafunzo hayo kuacha kutoa habari ambazo bado hujazithibitsha kutoka kwa vyanzo vyako .

Amewataka washiriki hao kuheshimu wahanga na waathirika kwani kufanya hivo ni jambo ambalo ni jema na litapelekewa kuaminika katika utendaji wa kazi zao.

Nao washiriki wa mafunzo wameihakikishia PACSO  kuyafanyia kazi mafunzo ambayo wameyapata kutoka kwa wakufunzi wao na kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa haki za binadamu.

Wamesema katika hili lazima mashirikiano yawepo ili kuondoa sintofahamu ambayo inaweza kujitokeza katika kazi zao.

Mafunzo hayo ya siku nne ambayo yamewashirikisha wadau mbali mbali wakiwemo waandishi wa habari ,wasaidizi wa sheria pamoja wadau wa habari kutoka kisiwani Pemba ,mafunzo ambayo  yameandaliwa na PACSO kwa ufadhili wa UNDP .