Loliondo FM
Loliondo FM
22 May 2025, 10:08 am

Wafugaji wengi wamekuwa wakivusha kifugo barabara kiholela bila kuzingatia kanuni za usalama barabarani kwa sababu mbalimbali ikiwepo kutojua kanuni za usalama barabarani.
Na Edward Shao
Jeshi la polisi kitengo cha usalama mkoa wa Arusha kwa kushirikina na wilaya ya Ngorongoro watoa elimu ya usalama barabarani .
Akitoa elimu hiyo ya usalama barabarani kupitia kipindi maalum na liliondo fm pamoja na mambo mengine mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Ngorongoro Erasto Kumburu ametoa elimu ya jinsi ya kuvusha mifugo barabara.
Amesema ili kuweza kuvusha mifugo lazima uangalie eneo ambalo unaweza ukaona umbali wa mita 100 na kwa kundi kubwa zaidi la mifugo inapaswa iwe na mtu zaidi ya mtu mmoja na endapo eneo halina alama wanaruhusiwa kutumia vitambaa vyekundu kufunga barabara kwa muda.
Kwa upande wake mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Rajabu Khatibu mkuu wa dawati la elimu ya usalama barabarani mkoa wa Arusha amesema endapo mfugaji atavusha mifugo barabara eneo lisilo sahihi ni hatari kwao pamoja na uharibufu wa miundombinu ya barabara.
Wilaya ya Ngorongoro ni miongoni wa wilaya zenye wafugaji wengi hivyo bado elimu ya kuvusha mifugo barabara inahitajika kutokana na kuwepo kwa barabara yenye kiwango cha lami ambayo imekuwa ikitumika pia kwa wafugaji hao kuvusha mifugo yao.