Vijiji vilivyokuwa vipimepigwa stop Ngorongoro ruksa kushiriki uchaguzi
16 September 2024, 3:36 pm
Baada ya kuwa na hofu na wasiwasi kwa wananchi wa baadhi ya vijiji, mitaa na vitongoji kutoshoriki uchaguzi ikiwepo wilaya ya Ngorongoro sasa watapata nafasi ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu.
Na mwandishi wetu.
Serikali kupitia ofisi ya Rais – TAMISEMI imevirejesha vijiji, kata na vitongoji ambavyo awali ilitangaza kuvifuta katika halmashauri za wilaya ya Ngorongoro kupitia tangazo namba 673 la Agosti 2, 2024.
Akizungumza hii leo jijini Arusha Septemba 16, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, Mhe. Mchengerwa amewaambia wanahabari kuwa kwenye orodha hiyo kumejumuishwa maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa tangazo la serikali ambayo pia yalihusisha tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ametangaza uamuzi huo wakati akiainisha vijiji 12,333, mitaa 4,269 na vitongoji 64,274 kupitia tangazo la serikali namba 769 linaloitaja mipaka ya vijiji vitakavyoshiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Aidha, Mchengerwa amewataka watanzania kujiorodhesha katika orodha ya wapiga kura kati ya Oktoba 11-20, 2024 na pia kujindaa katika kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo.