Wakinamama 1657 wamepewa elimu juu ya lishe Ngorongoro
20 December 2023, 10:57 am
Wilaya ya Ngorongoro ni moja ya wilaya ambazo wanaishi wafugaji kwa asilimia kubwa na chakula chao kikukuu ni nyama pamoja na maziwa hivyo maafisa lishe wamekuwa wakiendelea kutoa elimu juu ya kula lishe bora na faida zake katika jamii hiyo ya kifugaji.
Na Zacharia James.
Afisa lishe wa wilaya ya Ngorongoro Salum Ally Juma amesema jumla ya wakinamama wapatao 1657 wamepewa elimu juu ya lishe na uandaaji wa chakula cha nyongeza kwa watoto na upangaji sahihi wa mlo kamili unaozingatia makundi matano ya chakula katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha 2023/24.
Ameyasema hayo jumatatu ya Disemba 18/2023 wakati akisoma tathmini ya upimaji wa hali ya lishe kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wilayani hapa katika kikao cha kamati ya lishe ya Wilaya ambapo amesema akinamama hao waliopata elim hio wanatoka katika vijiji vya kipambi,Sakala,Olorieni,Lemishiri,Oldonyowas,maaloni,Irkanda,Tinaga na Lopoluni.
Katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2023 jumla ya watoto 34,290 wamefanyiwa upimaji ambapo watoto 31,789 sawa na asilimia 92.7 wanahali nzuri ya lishe,watoto 2,345 sawa na asilimia 6.8 wana hali hafifu ya lishe na watoto 156 sawa na asilimia 0.45 wana hali mbaya ya lishe.
Amebainisha kua kata na vijiji vyenye watoto wenye hali mbaya ya lishe ni Losoito katika watoto 576 watoto 25 wana hali mbaya ya lishe,Oloirobi katika watoto 496 watoto 6 wanahali mbaya ya lishe,Sukenya katika watoto 645 watoto 8 wana halimbaya ya lishe,Olorieni magaiduru(hospitali ya wilaya) katika watoto 2,976 watoto 35 wanahali mbaya ya lishe na Pinyinyi katika watoto 313 watoto 8 wana hali mbaya ya lishe katika kipindi hicho.