TADIO yawafikia wanahabari Loliondo
11 December 2023, 1:29 pm
Baada ya mtandao wa redio TADIO ambalo ni jukwaa linalounganisha redio za kijamii Tanzania kufanikisha mafunzo ya wanahabari ya namna yakuchapisha maudhui mtandaoni kwa Kanda ya kaskazini yaliyofanyika kwa siku mbili Desemba 7-8, 2023 sasa wameanza kuwapatia mafunzo wale waliosalia vituoni.
Na Edward Shao
Loliondo Fm ni miongoni wa redio wanachama wa TADIO ambapo wamefanikiwa kupata mafunzo kwa waandishi wao yanayohusu namna ya kuchapisha maudhui mtandaoni kupitia jukwaa maalum lilioanzishwa na TADIO linalojulikana kama radiotadio portal.
Mafunzo hayo yaliyotolewa na mhariri Bw. Hilali Ruhundwa kutoka TADIO yametolewa siku ya Jumatatu Desemba 11, 2023 katika ofisi za kituo hicho cha redio Loliondo Fm kilichopo makao makuu ya wilaya ya Ngorongoro Klkatika mji mdogo wa Loliondo yakiwa na lengo la kuwapa waandishi mafunzo ya namna ya kuchapisha maudhui mtandaoni ili habari zitakazokuwa zinatoka Ngorongoro ziwafikie watu wote sio tu ndani ya wilaya au taifa bali duniani kwa ujumla.
Bw. Ruhundwa amesama wao TADIO wamewafuata waandishi waliosalia vituoni kuhakikisha waandishi wote wananufaika na mafunzo hayo.
Kwa upande wake Bi, Rose Billas ambaye ni mwandishi wa habari na mnufaika wa mafunzo hayo kutoka Loliondo Fm amewashukuru TADIO kwa kuwapatia mafunzo hayo kwani amejifunza mengi kuhusu namna ya kuchapisha habari mtandaoni huku akitaja changamoto ya ufinyu wa vifaa ikiwemo kompyuta kuwapa wao ugumu katika kutekekeza kwa ufanisi kile walichofundhishwa.
TADIO wamekuwa wakiwapa mafunzo mabalimabali wanahabari wa redio wanachama wake na hata viongozi katika kuwajengea uwezo katika nyanja mbalimbali na imekuwa ikionesha na kutoa matokeo chanya kwa wanufaika hao.