Ngorongoro yanogeshwa na uhuru cup bonanza
10 December 2023, 6:37 pm
Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro imeadhimisha miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika kwa kuandaa mashindano ya mpira wa miguu yaliyokutanisha timu nne ambazo ni Serengeti boys,Loliondo sports,soitsambu fc na Merau fc.
Na Zacharia James
Timu Soitsambu fc wametawazwa kuwa mabingwa wa mashindano ya Uhuru cup bonanza 2023 mara baada ya kuwagaragaza waliokua mabingwa watetezi Serengeti boys ya waso magoli matatu kwa mawili katika mchezo wa fainali uliochezwa jumamosi tar 9/12/2023 katika uwanja wa waziri mkuu Pinda Wasso katika kusherehekea mia 62 ya Uhuru wa tanganyika.
Katika chezo huo magoli ya Soitsambu fc yalifungwa na mchezaji bora wa mashindano Bariki simon mawili dk za 12 na 32 na Omary john dk ya 59 huku ya Serengeti boys yakifungwa kwa mikwaju ya penati yote na kiungo wake machachali Kelvin erasto dk za 37 na 85,katika mchezo wa awali timu ya Loliondo sports wamefanikiwa kumaliza nafasi ya tatu mara baada ya kuwafunga Merau fc ya mugongo kwa mikwaju ya penati tano kwa nne mara baada ya kutoa sare tasa katika dakika 90 za mchezo huo.
Walio funga mikwaju ya penati kwa upande wa Loliondo ni Toni rashid,Jophu geofrey,Masanja gaidodi,Jonas john na Machete khamis na kwa upande wa Merau waliofunga ni kazi bengela ginishe maarufu kama shiboubu, Bonifas Jabuja mkulu,Baraka posta, na mlinda lango Ndunay tomasi katembo huku Yusufu bengela ginishe yeye alikosa .mshindi wa kwanza kajinyakulia Tsh.150,000,wa pili Sh.100,000 na watatu kaondoka na Sh.50,000.