Adhana FM

Othman Masoud : ACT_Wazalendo inafanya siasa zake kwa ueledi na maono makubwa

29 November 2026, 12:02 am

Mwenyekiti wa Chama cha ACT_wazalendo Taifa Othman Masoud Othman akizungumza katika mkutano wa Kamati kuu ya Chama hicho makao makuu Magomeni Dar es salaam

Na Rashid Kombo

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa Othman Masoud Othman amewataka wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kujadili kwa weledi maswala mbalimbali yanayowasilishwa mbele yao.

Othman ameyasema hayo Makao Makuu ya Chama hicho Magomeni Jijini Dar es Salaam alipofungua kikao cha kawaida cha Kamati kuu ya chama hicho pamoja na mambo mengine pia kutathimini hali ya kisiasa nchini, kupokea na kujadili taarifa za ziara mbali za viongozi na utekelezaji wa majukumu na shughuli za kawaida katika chama.

Aidha amewambusha viongozi hao kwamba ni vyema kuutumia kikamilifu uzoefu waliojijengea kwenye chama katika kuyakabili maswala ya kisiasa na kujamii katika kufikia malengo ya chama ya kuwatumikia watanzania.

Amesema kwamba chama hicho kinafanya siasa zake kikiwa na maono makubwa kwa kuelewa mahitaji ya Watanzania kwa kutumia njia sahihi za kutimiza matarajio ya wananchi hao kisiasa na kimaendeleo.

Naye Katibu Mkuu wa Chama hicho Ado Shaib Ado amesema kikao hicho ni cha kawaida na kimetimiza masharti yote ya kikatiba ikiwemo akidi ya kikao hicho.