Triple A FM

Babati? Labda msije

21 October 2024, 7:02 pm

Mchezaji bora wa mchezo Selemani Mwalimu akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli la pili

Na Joel Headman

Babati.

Ndio unavyoweza kusema kuwa njia pekee itakayokunusuru na kipigo hapa Tanzanite Kwaraa Babati ni wewe kutoleta timu yako uwanjani.

Maana ukiingiza tu kama utapona sana basi ni sare na waliobahatika kupata sare hapa dhidi ya Fountain Gate FC ni Dodoma FC pekee walipotoka sare maua ya magoli 2-2 Septemba 15.

Toka Fountain Gate walipotangaza uwanja huu kuwa wa nyumbani hawajapoteza mchezo wowote wa ligi kuu Tanzania Bara.

Leo ilikuwa zamu ya KMC mchezo uliopigwa saa 8 mchana na kushuhudia wana Kino Boys wakipokea kipigo kizito cha 3-1 huku wakimaliza pungufu baada ya mchezaji wao Ibrahim Elisa kupewa kadi nyekundu dakika za nyongeza za kipindi cha 1.

Kocha wa Fountain Gate FC Mohamed Muya amesema umoja ndani ya timu ndio silaha kubwa inayowabeba pamoja na jitihada za wachezaji.

Kocha wa Fountain Gate

Kwa upande wake kocha wa KMC Abdihamid Moallan amesema haikua mechi rahisi kucheza wakiwa pungufu toka kipindi cha kwanza na hali hiyo imewafanya kupokea kipigo hiko.

Kocha wa KMC

Kwa ushindi huo Fountain Gate wanakwea mpaka nafasi ya 2 ya msimamo wa ligi kuu chini ya Singida Black Stars ambao watavaana nao Ijumaa hii kwenye uwanja wa CCM Liti Singida kabla ya kurejea tena machinjioni Tanzanite Kwaraa Oktoba 28 kuwaalika wazee wa mapigo na mwendo Mashujaa fc ambao nao leo wametoa dozi ya 3-0 kwa Kengold pale Lake Tanganyika Kigoma.