Triple A FM
Triple A FM
28 October 2025, 10:55 am

“nimekutana na Kamati zote za usalama wilaya ndani ya Mkoa na tumejiridhisha kuwa kampeni zimeenda salama kwa amani na utulivu katika Majimbo yote na hali ya usalama katika Wilaya zote ni shwari.”
Na Furahini Jonas
Mkuu wa mkoa wa Arusha mh.Amos Makala amewahakikishai wananchi usalama kabla wakati na baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho Oct 29-2025
Makala amewasisitiza wananchi kudumisha amani na utulivu katika zoezi zima la uchaguzi na pia kujitokeza kushiriki zoezi hilo
Kwa upande mwingine mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Joseph Mkude amethibitisha kuwa vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya uchaguzi kwenye wilaya hiyo vimeshapokelewa na vipo tayari kwa matumizi ndani ya mitaa 154 na vituo 1051 vitakavyotumika kupigia kura
Wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla wenye sifa watashiriki zoezi la uchaguzi ambapo watapata fursa ya kuwachagua madiwani, Wabunge na rais kwa mujibu wa katiba ya nchi