Triple A FM

Mbinu kumlinda mtoto mtandaoni

17 October 2025, 2:02 pm

Bi Joseline Chambasi (aliyesimama) mtaalam kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi akizungumza na waalimu wa Shule ya Sekondari Arusha Day

Na Jackson Mbwambo

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imewataka wazazi na walimu nchini kuacha tabia ya kutoa uhuru mkubwa kwa watoto kutumia mitandao ya kijamii bila uangalizi, ikionya kuwa hali hiyo imekuwa chanzo cha kuongezeka kwa vitendo vinavyohatarisha maadili na usalama wao

Onyo hilo limetolewa wakati wa mafunzo ya usalama wa mtandao yaliyotolewa kwa walimu na wanafunzi wa shule mbalimbali jijini Arusha, ikiwemo Shule ya Sekondari Arusha Day, Arusha Sekondari, na St. Jude Sekondari Alhamisi tar.16-10-2025

Akizungumza katika mafunzo hayo Yusuph Kileo, mtaalam wa usalama wa mtandao, amesema wazazi wana jukumu la moja kwa moja katika kusimamia matumizi ya vifaa vya kielektroniki kwa watoto wao.

Sauti ya mtaalamu wa usalama usalama mtandaoni Yusuph kileo

Kwa upande wake, Joseline Chambasi, mtaalam kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, amewataka walimu kuwa makini na taarifa wanazochapisha mitandaoni, hasa picha na mahali walipo.

Mtaalam kutoka Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Josline Chambasi

Baadhi ya walimu waliopata mafunzo hayo walieleza kufurahishwa na elimu waliyoipata, wakisema imewasaidia kuelewa kwa undani umuhimu wa ulinzi wa taarifa binafsi na namna ya kuwa walinzi wa kwanza wa wanafunzi wao katika matumizi ya mitandao.

Sauti za waalimu

Mafunzo haya ni sehemu ya kampeni inayoendelea kitaifa katika kipindi cha Mwezi wa Kuadhimisha Usalama Mtandaoni, ambapo wataalamu kutoka wizara na taasisi mbalimbali wanazunguka mikoa tofauti nchini kutoa elimu ya usalama wa kidijitali kwa walimu, wanafunzi, na wazazi