Triple A FM
Triple A FM
16 September 2025, 4:38 pm

“Kuna baadhi ya wagombea ama vyama vya siasa vinaweza vikaja vikatoa sasa badae kwamba tunashukuru…”
Na Joel Headman
Kama haukuwa na taarifa kuna aina tofauti za rushwa hata zile ambazo hukuzisikia wala kudhani kama zipo.
Pengine unaweza kujiuliza ni ipi hiyo?
Hapa mkuu wa dawati la elimu kwa umma kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU mkoa wa Arusha bi Salome Swai anatufungua macho kuwa kuna rushwa ambayo huwenda ikatolewa kwa mtu kama shukrani
Miongoni mwa shukrani hizo ni Pamoja na ya kumshukuru mtu kwa kushiriki au kutoshiriki zoezi zima la uchaguzi
Anatufungua macho kuwa bado kuna aina nyingine ya rushwa ambayo mtu huweza kupewa kwa kusafirishwa kutoka sehemu moja Kwenda nyingine kwa ajili ya kupiga kura.
Lakini suala zima la kutoa magari,pikipiki au baiskeli kwa wananchi inaweza isiwe kitendo cha rushwa kutokana na mazingira na wakati vilivyotolewa