Triple A FM
Triple A FM
3 September 2025, 11:01 am

“Alafu ni mwendo kasi, sio kitu kingine ndio ajali ya pikipiki, ameingia mwenyewe”
Na Joel Headman
Afisa usafirishaji (bodaboda) mwanaume mkazi wa Arusha amejeruhiwa baada ya kupata ajali eneo la mataa ya kuongoza magari ya Triple A kwenye barabara kuu ya Arusha Nairobi jijini Arusha
Dereva huyo ambaye jina lake halijafahamika alikuwa akitokea Sakina kuelekea Mianzini kabla ya ajali hiyo iliyokatisha safari yake baada ya kuligonga kwa nyuma gari aina ya IST iliyokuwa imesimama kusubiri kuruhusiwa na taa
Kwa hali inayotajwa kuwa alikuwa kwenye mwendo kasi afisa huyo aligonga gari hilo kwa nyuma na kusababisha kioo cha gari kuvunjika na yeye kuingia ndani ya gari hilo
Hapa ni baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakielezea