Triple A FM
Triple A FM
3 September 2025, 10:48 am

Na Joel Headman
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Amos Makalla amewataka wananchi wa Wilaya ya Ngorngoro kuwa watulivu na kuendelea kudumisha amani na Mshikamano wakati wakisubiri majibu ya Tume mbili zilizoundwa kushughulikia changamoto zao.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Sale Kata ya Sale wilayani Ngorongoro amebainisha kuwa tayari ripoti ya tume mbili zilizoundwa na raisi zimeshakabisdhiwa na zitatolewa maamuzi baada ya uchaguzi mkuu wa 2025
Amewaomba viongozi wa kimila wa eneo la Ngorongoro kusaidia kudumisha hali ya Amani.
Rais Samia wakati alipokutana na Viongozi wa Jamii ya Kimasai Mkoani Arusha alitangaza kuunda tume mbili, Moja ikihusika na tathmini kuhusu masuala ya ardhi yanayolalamikiwa na wakazi wa eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na ya pili ilipewa kazi ya kuangalia utekelezaji wa uhamaji wa hiari kutoka eneo la hifadhi kwenda Msomera, Wilayani Handeni Mkoani Tanga