Triple A FM
Triple A FM
12 August 2025, 1:17 pm

Na Joel Headman
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Arusha wameomba kupatiwa elimu ya utambuzi wa habari za uongo na uzushi ili kuisaidia jamii kuwa salama na kujiepusha na migogoro ya kisheria.
Wakizungumza na Triple A fm leo mmoja wa wananchi hao John Omari ambaye ni mfanyabiashara katika soko la Kilombero ameeleza kukerwa na habari za uzushi ambazo zinazua taharuki katika jamii.
Katika jitihada za kutatua kero hiyo redio Triple A fm imemtafuta mtaalamu kutoka kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Africa inayojihusisha na utoaji wa mafunzo ikiwemo ya uthibitishaji wa habari kukabiliana na habari za uongo.
Mtaalamu huyu ni Daniel Samson ambaye ni mkuu wa mafunzo na utafiti wa Nukta Africa anaeleza kuwa kuna malengo tofauti ya mtu anayetoa taarifa za uzushi na uongo lakini pia kuna namna kadhaa za kukabiliana nazo