Triple A FM
Triple A FM
2 June 2025, 10:31 am

Na Joel Headman
Asasi za kiraia nchini Tanzania zinatarajia kuanza maadhimisho ya wiki ya AZAKI 2025 (CSO Week 2025) itakayo jadili Dira ya maendeleo ya Taifa pamoja na kuwakutanisha wadau na washiriki wasiop[ungua 800
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya AZAKI na Mkurugenzi Mkazi wa CBM International Tanzania Nesia Mahenge amesema tukio hilo litafanyika kuanzia tarehe 2 hadi 6 Juni 2025 katika Hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha
Ametaja tukio hilo kuwa la umuhimu kutokana na kuwa na fursa ya kutathimini safari ya pamoja katika kushughulikia changamoto za ndani, na kuandaa mikakati ya pamoja kwa ajili ya maendeleo ya taifa
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya FCF na Rais wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Mercy Sila, ametoa rai kwa vijana na Wanawake kushiriki na kutoa maoni yao kuhusu masuala ya maendeleo.
Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS) Justice Rutenge amesema kuwa CSO Week 2025 ni tukio la kitaifa linalotoa fursa kwa Watanzania kushiriki katika kutoa maoni yao kuhusu Dira ya maendeleo 2050.