Triple A FM

Kibano kwa madereva wa serikali

26 May 2025, 10:18 am

Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed

Na Joel Headman

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha limetoa mafunzo kwa madereva wanaondesha magari ya Serikali mkoani hapa kwa ajili ya kuwajengea uwezo juu ya matumizi sahihi ya barabara na mifumo ya Jeshi la Polisi

Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema mafunzo hayo ni muendelezo wa kuyafikia makundi mbalimbali katika jamii kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika kukabiliana na ajali za barabarani na kufahamu mifumo mipya ya Jeshi la Polisi katika kufuatilia haki zao.

SSP Zauda amebainisha kuwa Jeshi la Polisi linamifumo mingi katika kutekeleza majukumu yake ambapo madereva wamepata fursa ya kujifunza mifumo mbalimbali ikiwemo mfumo wa ukaguzi wa magari, mfumo wa leseni na mfumo wa ukaguzi wa madeni ya Serikali.

Mkuu wa Polisi Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed

Akizungumza kaimu Meneja wa Mamlaka ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi OSHA kanda ya Kaskazini Abubakari Shabani amesema wamepata fursa ya kutoa elimu juu ya umuhimu wa kupima afya hususani macho na kueleza kuwa itasaidia kupunguza ajali zinazoweza kutokea kutokana na changamoto ya uoni.

Miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo wameshukuru na kuahidi kuwa yatawaletea mabadiliko katika utendaji kazi wao.

Baadhi ya wanufaika wa mafuzo