Triple A FM
Triple A FM
12 May 2025, 11:48 am

Katika hali isiyotarajiwa Mh. Mrisho Gambo amerusha jiwe gizani katika mkutano wake wa hivi karibu
Na Joel Headman
Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo amezidi kuweka utata kwenye suala la ujenzi wa jengo la utawala la jiji la Arusha lililokwama toka mwaka 2019.
Utata huo umeibuliwa na Gambo mwenyewe kwenye mkutano wake wa hadhara alioufanya kwenye eneo la soko kuu jijini hapa kuhusu ahadi na utekelezaji alioufanya ndani ya miaka mitano ya ubunge wake.
Gambo ameeleza kuwa bado kuna utata katika ujenzi wa jingo hilo na kuwa ataendelea kulisemea ili kuhakikisha mambo yanafanyika kama yalivyokusudiwa.
Itakumbukwa kuwa mbunge Gambo aliibua hoja hiyo bungeni wakati alipomtuhumu waziri wa wanchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa kuwa amesema uongo wakati akitoa maelezo ya serikali dhidi ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa jingo hilo.
Tuhuma hizo zilimlazimu spika wa bunge Dk. Tulia Ackson kuagiza jambo hilo lichunguzwe na kamati ya kudumu ya haki, maadili na madaraka.
Hata hivyo kabla ya utekelezaji wa agizo hilo, tarehe 23/04/2025 Gambo alisimama bungeni kuomba radhi na kufuta maneno aliyokuwa ameyatoa dhidi ya waziri Mchengerwa.