Triple A FM

Wali wachoma vyumba 7 Arusha

2 May 2025, 11:30 am

Na Joel Headman, Arusha

Vyumba 7 vimeungua kwa moto kwenye mtaa wa Jordan kata ya Kiutu mkoani Arusha baada ya kushika moto uliotokana na jiko la gesi.

Moto huo ulioanzia kwenye chumba cha mkaazi mmoja wa eneo la Jordan unadaiwa kutokea baada ya mototo mdogo kuwasha jiko la gesi ili kupasha chakula.

Mtoto huyo ameeleza kuwa alibaki mwenyewe nyumbani na alipohisi njaa aliamua kupasha chakula ili ale.

Mtoto

Akizungumza katika eneo la tukio Gervas Mose ambaye ni jirani wa nyumba iliyoungua anasema mida ya mchana walisikia watoto wakicheza na baada ya muda pakawa na utulivu kabla ya moto kuanza.

Gervas Mose

Kwa upande wake Angelina Karani ambaye ni mkazi wa eneo hilo amewatahadharisha wazazi kuwa karibu na watoto ili kuepusha madhara ya aina hiyo.

Bi Angelina Karani