Triple A FM
Triple A FM
1 May 2025, 12:48 pm

Na Joel Headman, Arusha
Baadhi ya waumini na mchungaji wa kanisa la Wanafunzi wa Yesu Kristo Tanzania lililopo Kijiji cha Ilkiding’a mtaa wa Laiza kata ya Ilikiding’a Mkoani Arusha na baadhi ya waumini wamejikuta katika hali ya sintofahamu baada ya kushambuliwa wakiwa kwenye ibada ya asubuhi (Morning Glory)
Akizungumza mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Alphonce Mallya ameeleza kuwa wakati wakiendelea na ibada ya Morning Glory alishangaa kumuona mtu aliyejitambulisha kuwa ni mgambo akifungua vyombo vya muziki na kumfunga pingu kasha kushambulia waumini.
Bi Enoti Musa ambaye ni muumini aliyepigwa na mtu huyo ameeleza kuwa chanzo cha kupigwa kwake ni kujaribu kutoa simu ili kuwapigia waumini wengine kuja kutoa msaada.
Mmoja wa wananchi wa mtaa wa Kioga Joshua Laizer ambaye pia ni mgambo ameeleza kuwa mtu huyo aliyefanya tukio hilo anapaswa kujitokeza na kuomba radhi kwani bila kufanya hivyo ataandamwa na laana.
Endelea kufuatilia vipindi na habari zetu wakati jitihada za kutafuta jeshi la polisi mkoa wa Arusha zikiendelea