

31 January 2025, 10:29 am
Na Joel Headman, Arusha
Wananchi wa Arusha wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni juu ya maandalizi ya dira
mpya ya maendeleo ya taifa mwaka 2050.
Wito umetolewa na hakimu mkazi wa mahakama ya Arumeru mkoani hapa Theresia Sedoyeka wakati wa utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu mausala mbalimbali kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria ikiwemo maandalizi ya dira ya taifa ya maendeleo
ya mwaka 2050.
Amesema wananchi ni nguzo muhimu katika maandalizi ya dira hivyo wanahamasishwa kujitokeza kuchangia maoni.
Hakimu Theresia Sedoyeka
Kwa upande wake wakili wa kujitegemea Castro Shirima ameeleza kuwa licha ya wananchi kutoa
maoni ya dira lakini pia watanufaika na elimu ya sheria inayotolewa bure.
Wakili Castro Shirima
Wiki ya sheria hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuhitimisha mwaka wa shughuli za kimahakama na kuanza mwaka mpya ambapo kwa mwaka huu yameanza Januari 25 na yanatarajiwa kuhitimishwa leo Januari 31 yakifuatiwa na kilele cha siku ya sheria nchini tarehe 3 Februari 2025
Maadhimisho ya mwaka huu yanabebwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania 2050 Nafasi ya taasisi zinazosimamia haki madai katika kufikia malengo makuu ya taifa ya maendeleo”